Bondia wa ngumi za kulipwa Hassan Mwakinyo anatarajia kupanda ulingoni dhidi ya Mkenya, Rayton Okwiri kuwania mkanda wa kimataifa wa ‘IBA’ katika pambano ambalo litafanyika Septemba 29, mwaka huu.

Mwakinyo atapanda katika pambano hilo ambalo limeandaliwa na Kampuni ya Promosheni ya Ngumi za Kulipwa nchini ‘PAF Promotion Company LTD’ ikiwani pambano lao la pili tangu waingie katika mchezo wa ngumi za kulipwa.

Kwa mujibu wa Chama cha Ngumi za Kulipwa za Kimataifa ‘IBA’ kimetangaza taarifa ya Mwakinyo kupanda ulingoni na Okwiri katika pambano la kuwania ubingwa wa mabara wa ‘IBA’ kwenye uzani wa Walter.

‘IBA’ imesema kuwa, Mwakinyo atapanda ulingoni kwenye pambano hilo akiwa anakamata nafasi ya 70 duniani wakati mpinzani wake akiwa ni Bondia wa 200 duniani.

Katika pambano hilo ambalo msimamizi wake na mwakilishi wa ‘IBA’ atakuwa ni Stephane Cabrera raia wa Ufaransa huku mratibu akitarajia kuwa ni Emmanuel Mlundwa akisaidiwa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini ‘TPBRC’.

Greenwood aziingiza vitani Italia, Saudi Arabia
Spurs yamtega Romelu Lukaku