Baada ya kuwepo taarifa za kutaka kurejea katika klabu yake ya zamani, aliyekuwa kocha msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi amesema hana mpango wa kurudi tena Mbeya City ambayo aliipandisha daraja.
Kocha Mwambusi alitajwa kuwa miongoni mwa makocha wanne walioomba kufundisha timu hiyo, lakini amesisitiza kuwa hakuna ukweli wa jambo hilo kwa vile hana mpango huo kwani ameamua kupumzika kujihusisha na masuala ya soka kwa sasa
“Sina mpango huo, watu wametaja kuwa ningefundisha timu nyingi lakini nimeamua kupumzika kwa sasa hivyo hakuna ukweli wowote kwamba nimeomba kazi ya kuifundisha Mbeya City, sijafikiria hivyo kabisa, ” alisema Mwambusi.
-
Hizi ndio sababu zilizo mkimbiza kocha wa Njombe Mji
-
Simba yashindwa kuunguruma CCM Kirumba, yabanwa na Mbao
-
Wagonga nyundo wa London washindwa kutamba mbele ya Spurs
Mapema mwezi Julai Juma Mwambusi aliachana na Yanga baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa misimu miwili na kuipa mafanikio makubwa ikiwemo kutwaa mataji mawili ya ligi ya Vodacom na kombe moja la FA.
Mbeya City kwa sasa inashika nafasi ya 7 katika msimamo wa ligi kuu ya Vodacom ‘VPL’ baada ya kucheza michezo minne.