Haki Elimu kupitia Mkurugenzi wake, Dk John Kalage wamesema huenda kukafanyika mabadiliko kwenye suala zima la elimu hususani juu ya lugha zinazotumika kufundishia na kujifunza katika ngazi mbalimbali za elimu hapa nchini.

Hayo yamezungumzwa kufuatia mjadala ulioandaliwa na Haki Elimu uliowahusisha wahadhiri mbalimbali kutoka ngazi mbalimbali za elimu ambapo mada kuu iliyokuwa inazungumzwa ni juu ya mchango wa lugha ya kufundishia na kujifunza katika kuufikia uchumi wa kati ifikapo 2025”.

Ambpao Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu Kishiriki cha Ualimu Dar es salaam (DUCE), akichangia hoja amesikika akisema mwanafunzi wake mmoja amejibu maswali ya mtihani wa kingereza kwa kutumia lugha ya Kiswahili licha ya mtihani huo kuelekeza majibu yatolewe kwa lugha ya kiingereza  jambo ambalo limewaweka wakufunzi wake njia panda.

Amesema ”Juzi tumekutana na kihoja kuna mwanafunzi mmoja ambaye maswali yote amejibu kwa Kiswahili na mtihani ni wa kingereza, mpaka sasa hivi tunajadiliana kwamba tutafanya vipi maana sera hairuhusu. Hivyo utaona kwamba kuna shida mahala fulani na hata wanafunzi wetu ukiangalia insha zao ni tatizo”.

Licha ya Sera ya 2014 inayotaja lugha ya kiswahili na kiingereza kuwa ni lugha rasmi za kujifunzia lakini kiswahili kinatumika kufundishia elimu ya awali na msingi wakati kiingereza kinatumika kufundishia katika baadhi ya shule za msingi huku kikiwa ni lazima kwa sekondari, vyuo vya ualimu, vyuo vya yfundi na elimu ya juu.

Aidha mchangiaji mmoja wa mada hiyo amesema lugha ya kingereza ni tatizo kwa wanafunzi wengi hapa nchini hivyo amependekeza kuwepo na progamu maalumu itakayotumika kufundishia lugha ya kiswahili na si kufundisha Historia kwa kingereza kwa lengo la kutaka wanafunzi hao kujua kingereza.

 

Kumbilamoto: Mgogoro wa CUF ni sawa na ule wa Israel na Palestina
Gareth Bale amkuna meneja mpya Real Madrid