Aliyekuwa Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa kata ya Vingunguti kwa tiketi ya CUF, Omary Kumbilamoto ameamua kujiuzulu nafasi hiyo na kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais John Pombe Magufuli.

“Nimejivua uanachama wa CUF na nafasi zangu zote ndani ya chama ikiwemo ya udiwani katika kata ya Vingunguti pia unaibu meya wa manispaa na nimechukua hatua hii ili kulinda na kutetea maslahi ya wananchi ninaowatumikia hivyo ili niendelee kutekeleza majukumu yangu ipasavyo najivua ili kuunga mkono jitihada za rais Magufuli na viongozi wote Serikali kwa ujumla” amsema Kumbilamoto.

Aidha amesema kuwa kwa sasa ataendelea na shughuli zake za kilimo mpaka pale atakapoamua kuwajulusha wananchi chama gani atachoamua kujiunga upya.

Video: Ngome ya Lowassa yatikiswa, Chadema yazidi kumeguka
Jose Mourinho aiponda ziara ya Marekani