Mamlaka za nchi ya Panama zimemkamata na kumshikilia mtu mmoja aliewahi kuhudumu kama mwanajeshi nchini Colombia akitakiwa kuhojiwa kwa kuhusika na kifo cha aliekuwa Rais wa Haiti, Jovenel Moise.
Vyanzo vya habari vinasema, Mtuhumiwa huyo, Mario Antonio Palacios, 43, alikamatwa siku ya Jumatatu katika kituo kimoja cha ndege alipokua akitokea Jamaica kuelekea Colombia.
Gazeti la “The standard” linaripoti kuwa mamlaka za Haiti zinamshikilia Palacios kwa kuunda kikundi cha mauaji ambacho kilihusika kumuua Rais Moise July mwaka jana nyumbani kwake na kumjeruhi mke wake.
“Palacios alizuiliwa katika kituo cha ndege Panama na kutakiwa na mamlaka kupanda ndege kwa hiari inayoelekea Amerika,” alisema mfanyakazi wa uhamiaji wa Colombia.
Taarifa zinasema kuwa Haiti tayari imeitisha taarifa zote za upelelezi kutoka shirika la kimataifa la upelelezi la ‘Interpol’ ili kuendelea kuwa na uhakika wa kila hatua aliyoichukua Palacius.
Hata hivyo vyombo vya habari vya Haiti vimezuiliwa kutoa habari zozote kuhusu tukio hilo kwa sasa mpaka katua zote za kiuchunguzi zitakapokamilika ikiwa ni pamoja na vyomo vya ulinzi na usalama vya nchi hiyo kuanzia maafisa wa uhamiaji hadi polisi.
Rais wa Haiti Jovenel Moise aliuawa July 1, 2021 katika shambulio dhidi ya makazi yake mjini Port-au-Prince na watu wasiojulikana waliojihami kwa silaha saa 01:00 saa za eneo hilo ikiwa ni saa 11 alfajiri kwa saa za Afrika Mashariki.