Mwanamazingaombwe maarufu nchini India Chachal Lahiri (47), maarufu kama “Jadugar Mandrake”, anahofiwa kufariki dunia baada ya kujaribu kuigiza muujiza wa kuruka mtoni akiwa amefungwa mikono na miguu, na kutumbukizwa kichwa chini miguu juu.

Imeelezwa kuwa jana majira ya mchana alifungwa mikono na miguu kwa minyororo ya chuma na kuzamishwa mtoni kwa kutumia boti huku umati wa watu ukimshuhudia jinsi atakavyo jifungua na kutoka mtoni humo.

Binamu yake Rudra Prasad ameliambia shirika la News 18 kuwa ” ilikuwa ni sehemu ya maonyesho aliingia mtoni huku mikono yake na miguu ikiwa imefungwa, alifanikiwa kujifungua lakini punde mawimbi yakaongezeka na akazama. bado tumechanganyikiwa hatujui ilitokeaje”

” Mwili wake bado haujapatikana, bado tupo katika hali ya taharuki, alikuwa mwanamazingaombwe makini, amefanya vitendo vya kuzama majini mara nyingi lakini aliibuka, aliwekeza maisha yake yote kwenye maigizo ya viini macho” aliongeza Prasad.

Lahiri ni mkazi wa mjini Sonarpur, ana mtoto mmoja wa kiume (15). rafiki zake na majirani pamoja na uongozi wa serikali za mitaa wameelezea jinsi walivyopokea kwa mshtuko taarifa hiyo.

Mnamo mwka 2013, mwanamazingaombwe huyo alizomewa na mashabiki wake alipofanya onesho kama hilo baada ya kuhisi amewadanganya.

Polisi na kikosi cha wapiga mbizi wamepiga doria katika eneo hilo lakini hadi kufika jioni walikuwa hawajafanikiwa kumpata Lahiri, na Afisa mmoja amelieleza gazeti la Hindustan Times kwamba mpaka mwili wake utakapo patikana, ndipo atakapo thibitishwa kuwa amefariki.

Mmoja ya walioshuhudia tukio hilo ni mpiga picha wa gazeti Jayant Shaw, amesema kwamba kabla hajaingia mtoni mwanamazingaombwe huyo alizingumza naye.

“Nilimuuliza kwanini una hatarisha maisha yako kwa kiini macho, ” Lahiri alitabasamu na kusema, ‘Nikifanikiwa ni miujiza, nisipofanikiwa basi litakuwa janga” alieleza Shaw.

 

Tanzania kinara wa Amani nchi za Afrika Mashariki
Makonda atimiza ahadi yake kwa klabu ya Yanga