Aliyekuwa Mshambuliaji wa Simba SC Mghana, Augustine Okrah amejiunga na Klabu ya Bechem United ya nchini Ghana.

Mghana huyo ni kati ya wachezaji walioachwa na Simba SC katika msimu huu, baada ya kuingia makubaliano mazuri kwa pande hizo mbili, mchezaji na klabu ya kuuvunja mkataba wa mwaka mmoja.

Kiungo huyo tangu ajiunge na Simba SC, hakuwa na msimu mzuri kutokana na kusumbuliwa na majeraha kila mara kabla ya kuvunjwa mkataba wake na kurejea kwao Ghana.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika moja ya jarida kubwa la nchini humo, limeripoti kuwa kiungo huyo ameingia makubaliano ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja.

Kiungo huyo baada ya kusani mkataba huo, alitambulishwa kwa mashabiki huku akikabidhiwa jezi namba 10 aliyokuwa anaivaa kabla ya kutua Simba SC.

“Okrah rasmi amerejea katika klabu yake ya zamani ya Bechem aliyokuwa anaichezea kabla ya kujiunga na Simba SC katika msimu uliopita.

“Amejiunga na klabu yake hiyo kama mchezaji huru baada ya kuvunja mkataba wa mwaka mmoja na Simba SC ambayo haikuwa na mpango na kuendelea naye,” liliandika Jarida hilo.

Jadon Sancho kutafuta suluhu Man Utd
Xavi Hernandez hadi mwaka 2025