Mahakama nchini Rwanda, imemkuta na hatia Moise Emmanuel Bagirishya ambaye alishitakiwa kwa mauaji ya kumgonga na gari hadi kufa bila kukusudia, Mhariri wa gazeti la The Chronicles, John Williams Ntwali.

Katika hukumu hiyo, Dereva huyo alipewa adhabu ya kulipa faini ya faranga milioni moja za Rwanda, sawa na dola 920 kwa kosa hili la kifo cha mwanahabari mashuhuri ambaye alikuwa mkosoaji wa serikali.

Siku ya tukio, Januari 18 2023 Dereva Birigisha alikuwa akiendesha gari kwa kasi na kupelekea kugonga pikipiki iliyokuwa inamsafirisha Ntwali na kupelekea umauti wake.

Mhariri wa gazeti la The Chronicles, Marehemu John Williams Ntwali. Picha ya The Globe and mail.

Mbele ya Mahakama jijini Kigali, Birigisha alikiri kosa na aliomba msamaha kwa ajali hiyo n akusema, “nilimuua Ntwali wakati nilipokuwa nikiendesha gari kwa kasi na nikiwa nimechoka,” na kesi hiyo ilifuatiliwa na wanahabari wachache walioalikwa kusikiliza hukumu.

Ntwali, ambaye alikamatwa mara nyingi katika miongo miwili ya kazi yake ya uandishi wa habari, alikuwa anamiliki televisheni ya Pax kwenye mtandao wa YouTube, ambayo ilikuwa imejidhihirisha kama chombo cha habari pekee kinachoripoti habari za kusimumua nchini Rwanda.

Mexime aichimba mkwara Kagera Sugar
Edo Kumwembe aipeleka Young African Robo Fainali