Mwandishi wa Habari za Michezo na Mchambuzi Mwandamizi Edo Kumwembe, anaamini Kikosi cha Young Africans kina kila sababu ya kufanya vizuri katika Michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika msimu huu 2022/23.

Young Africans itaacheza mchezo wa kwanza Hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Barani Afrika Jumapili (Februari 12) dhidi ya US Monastir ya Tunisia.

Akizungumza kwenye Kipindi cha Michezo cha Sports Arena cha Radio Wasafi FM mapema leo Jumatano (Februari 08), Edo amesema msimu huu Young Africans ina kikosi Bora na Imara, tofauti na ilivyokuwa msimu uliopita, hivyo anatarajiwa kuona wakifika mbali kwenye michuano hiyo.

“Huu ni wakati mzuri kwa Young Africans kushiriki hii Michuano maana hawana ‘excuse’ yeyote, wana Wachezaji wazuri na wenye experience huu ndio muda kuonesha uwezo wao”

“Ile Young Africans ya Miezi 36 iliyopita ingepata shida sana lakini nikiiangalia hii ya sasa wakijikamua kidogo tu wanafika Robo Fainali” amesema Edo Kumwembe

YoungA fricans ilitinga Hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Barani Afrika, baada ya kuifunga Club Africain 0-1, nyumbani kwao Tunis-Tunisia, baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana jijini Dar es salaam.

Mwandishi afariki kwa ajali, dereva ajitetea
Ahmed Ally: CAF imetupa masharti maalum