Mwandishi wa habari za uchunguzi aliyesaidia kufichua uwepo wa rushwa kwenye Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) ameuawa kwa kupigwa risasi katika mji mkuu wa Ghana Accra.

Ahmed Husein ni miongoni mwa wanahabari walioshiriki katika uchunguzi wa mwenendo wa uongozi wa mpira wa miguu Afrika, ambapo habari zao ziliwakilishwa na Anas Aremeyaw aliyeshinda tuzo.

Katika habari zao za uchunguzi zilipelekea kiongozi wa juu wa mpira wa miguu nchini Ghana kujiuzuru na viongozi wengine wengi wa mpira wa miguu walitumbuliwa.

Msemaji wa polisi jijini Accra amesema kuwa mwandishi huyo alipigwa risasi shingoni na kifuani na mtu asiyejulikana alipokuwa anaelekea nyumbani kwake jana usiku.

Mwandishi mwenzie aliyefanya naye upelelzi huo Anas ameandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa kijamii kuwa ” habari ya huzuni, lakini hatuta nyamazishwa. pumzika kwa amani Ahmed”

Aidha, ikumbukwe kuwa mwezi wa kumi mwaka jana shirikisho la mpira wa miguu Duniani (FIFA), lilimuondoa Madarakani kiongozi mkuu wa mpira wa miguu, Kwesi Nyantakyi na kumtoza faini ya dola 500,000 baada ya kamera kumnasa akipokea rushwa.

Hata hivyo, katika hatua nyingine marefa 8 na wasaidizi wao walifungiwa kujihusisha na mpira wa miguu milele, na maofisa wengine 53 walifungiwa kwa miaka 10.

 

 

 

 

Abiria 36 watekwa nyara Cameroon
Tundu Lissu auota urais 2020, atakayeamua siyo Lowassa