Hatimaye Balozi Juma Mwapachu amerudisha kadi ya Chama Cha Mapinduzi aliyokuwa nayo tangu chama hicho kilipoanzishwa mwaka 1977.

Balozi Mwapachu amerudisha kadi hiyo leo katika ofisi za CCM, Mikocheni, Dar es Salaam na kumkabidhi Katibu wa Siasa na Uenezi CCM, Mtaa wa Mikocheni A, Sudi Odemba.

Balozi Mwapachu alitangaza kuihama CCM na kutojiunga na chama chochote bali upande aliouita wa ‘Mabadiliko’, akidai kuwa chama hicho kilivunja katiba yake katika mchakato wa kumpata mgombea urais na kwamba kimepoteza dira.

Akizungumzia uamuzi wake, Balozi Mwapachu alisema kuwa hali ilivyo sasa katika CCM, hata Mwalimu Julius Nyerere angekuwepo angekihama chama hicho.

Lowassa: Hakuna Wa Kutuzuia…
TFF Yakamilisha Maandalizi Ya Yanga Vs Azam