Mkoa wa Mtwara leo Agosti 28, umepokea Mwenge wa Uhuru ukitokea Lindi ambapo Mwenge huo umewasili Mtwara majira ya saa moja asubuhi na kupokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Dunstan Kyobya Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Brigedia Jenerali, Marco Gaguti.
Aidha Mwenge huo utakimbizwa katika wilaya tano kuanzia leo Agosti 28, hadi Septemba 1, 2021 na kukabidhiwa mkoani Ruvuma Septemba 2, 2021.
Akitoa taarifa mara baada ya kuupokea mwenge huo katika Kijiji cha Mpapura, Kyobya amesema Mwenge wa Uhuru utakimbizwa kwenye njia ya urefu wa kilomita 556 na kupitia jumla ya miradi 42 yenye thamani ya zaidi ya shiling bilioni kuni na moja, milioni mia na laki mbili.
Aidha pamoja na kazi nyingine Mwenge utaweka mawe ya msingi miradi nane, kufungua miradi tano, kuzindua miradi Saba, kuona na kukagua miradi 22 inayotekelezwa na wananchi kwa kushirikiana na Serikali, wahisan na wilaya.