Jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam linamshikilia Mohamed Jumaa Lardh (37) mkazi wa Kariakoo  kwa tuhuma za kuwaua walinzi  wawili eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam.

 Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda maalumu ya  Dar es Salaam Muliro Jumanne, ametoa taarifa hiyo kwenye vyombo vya Habari leo Agosti 27, 2021.

Muliro amesema kuwa tukio hilo limetokea Agosti 26 maeneo ya Tungi Wilaya ya Kigamboni, mtuhumiwa amewaua Eliakim Morali (30) mkazi wa Mbezi Beach na  Saunko Bakari (35) mkazi wa Buguruni  walinzi wa Kampuni ya Lock Fort Security.   

Mohamed anadaiwa kuwagonga na kuwaua kwa makusudi walinzi hao na Lori lenye namba za usajili T 176 CYP, huku watu watano wakijeruhiwa kwenye tukio hilo.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani hivi karibuni kujibu tuhuma zinazomkabili.

Maaskari waliouawa kwenye shambulio la risasi Dar waanga leo
Joe Biden atangaza kiama kwa waliolipua bomu