Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Ummy Mwalimu, amezitaka Halmashauri 11 nchini kutoa maelezo kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI ndani siku 14, ni kwa nini wametekeleza mpango wa Lishe kwa kiwango cha asilimia 25.

Ametoa maaagizo hayo, leo Agosti, 26, 2021, wakati akifungua Mkutano wa Tano wa Kupitia Afua za Lishe, unaofanyika mkoani Shinyanga katika Manispaa ya Kahama, ambapo amesema lengo la Serikali nikuona nchi inaondokana na suala la uatapiamlo na udumavu kwa wananchi wake.

Aidha Halmashauri hizo ni pamoja na Halmashauri za Wilaya ya Tarime, Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, Wilaya ya Sikongwe mkoani Tabora, Wilaya ya Chato mkoani Geita, Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Wilaya ya Ileje mkoani Mbeya, Wilaya ya Itigi mkoani Singida, Halmashauri ya Manispaa ya Musoma,  Handeni Mji mkoani Tanga,  Shinyanga mkoani Shinyanga, na  Manispaa ya Tabora mkoani Tabora.

Pamoja na hayo Waziri Ummy amewapongeza Wakuu wa Mikoa kwa kuhakikisha ongezeko la utoaji ya fedha kwa ajili ya kutekeleza afua za lishe, kutoka asilimia 22 kwa mwaka wa fedha 2017/18, asilimia 52 kwa mwaka wa fedha 2019/20 na kufikia asilimia 57 kwa mwaka wa fedha 2020/21.

Amesema kuwa Ongezeko hilo la utoaji wa fedha ni mabadiliko chanya katika kutekeleza afua zingine zinazotegemea kiashiria cha kupanga na kutumia fedha katika Halmashauri, huku akitaka kuongezwa juhudi zaidi ili kukidhi kile walichokubaliana shilingi 1000 kwa kila mtoto chini ya miaka mitano.

TPRI yakamata kiuatilifu bandia chupa 140
Rais Samia apokea hati za utambulisho wa Mabalozi 5