Zikiwa zimepita chache baada ya Bunge la Uganda kuamuru uchunguzi ufanyike kuhusiana na madai ya kuhamasisha vitendo vya mapenzi ya jinsi moja mashuleni, mmiliki wa nyumba jijini Kampala amemfukuza mpangaji wake kutokana na tuhuma za kujihusisha na vitendo hivyo.

Hatua ya bunge ilitokana na ujumbe wa video uliokuwa ukizunguka katika mitandao ya kijamii mwezi uliopita ukimwonesha mtu mmoja aliyejitambulisha kwa jina Eric Ndawula ambaye ni mkazi wa Kampala kuwa shoga.

Ndawula mwenye umri wa miaka 26, alisema mwenye nyumba wake alimwonesha video hiyo iliyowekwa kwenye mtandao na mtu asiyejulikana, na kisha kumpa notisi ya kumfukuza kwenye nyumba akisema kuwa nyumba yake haipangishwi kwa mtu anayejihusisha na mapenzi ya jinsi moja.

“Mimi kwa sasa nimekuwa tishio katika jamii hususani kwa watoto wanaonizunguka kwa sababu wataniiga na kujihusisha na mapenzi ya jinsi moja,” alisema Ndawula huku akijutia hali hiyo iliyosababisha kufukuzwa katika nyumba aliyopanga.

Mafuriko yaua wanne Malaysia 40,000 wakimbia makazi
TRC wapongeza maendeleo mradi wa JNHPP