Mwanaume mmoja jijini Birmingham nchini Uingereza amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Weymouth (Weymouth Magistrates’ Court) kwa kosa la kufanya mapenzi na mkewe mbele ya nyumba ya jirani yao, baada ya kukasirishwa na kitendo cha jirani huyo kumkatalia kuegesha gari kwenye eneo hilo.

Katika maelezo yaliyowasilishwa Mahakamani hapo, Lee Craig McConnell (28) alikuwa na tabia ya kuegesha gari mara kwa mara mbele ya nyumba ya jirani yake. Jirani huyo alimkataza mara kadhaa kuegesha gari katika eneo hilo, lakini aliendelea.

Kwa mujibu wa Dorset Live, ili kuzuia hali hiyo, jirani alilazimika kuweka kizuizi (bollard) ili McConnell asiweze kuweka gari lake kwenye eneo hilo la wazi lililo mbele ya nyumba yake. Jirani huyo alienda mbali na kufunga CCTV Camera kuhakikisha anaona kila kinachoendelea.

Ilielezwa kuwa majira ya saa tano usiku, Oktoba 2022, CCTV Camera zilinasa tukio, ambapo mtuhumiwa alionekana akifika katika eneo hilo, kwanza akavua nguo na kujichua huku akielekea kwenye kamera. Kisha, alimuita mkewe ambaye alikuja akiwa amevalia gauni la kulalia na wakaanza kufanya mapenzi.

Mlalamikaji alieleza kuwa kitendo kile kililenga kumdhalilisha, kumtisha na kumfedhehesha kutokana na mgogoro uliokuwepo kati yao.

Wakili wa mtuhumiwa, Simon Lacey aliieleza Mahakama kuwa mtuhumiwa ambaye alikiri kosa, amesikitishwa na kitendo hicho ambacho kimekuwa zaidi ya somo kwake kwani ana familia na Watoto.

“Amepata fedheha kubwa sana na amejifunza somo gumu ambalo limeacha alama kwenye maisha yake,” alisema Simon Lacey.

Alisema mshtakiwa huyo yuko kwenye wakati mgumu kisaikolojia kwani hadi sasa video iliyonaswa na CCTV kamera anayo mlalamikaji na hajui itakuwaje siku za usoni.

Aidha, aliiambia Mahakama kuwa mteja wake ameamua kuhama katika eneo hilo ili kuepuka fedheha na aibu kutokana na vitendo vyake, na kwamba amebadilika.

Baada ya kusikiliza maelezo ya pande zote mbili, Mahakama iliahirisha kesi hiyo hadi Aprili 27, 2023. Ilimuachia mshtakiwa kwa dhamana na kuweka zuio la kutomsogelea au kuwasiliana na mlalamikaji.

Maeneo ya kazi 1,588 yaonja chungu ya OSHA
Adel Amrouche akabidhiwa mikoba Taifa Stars