Serikali imesema kuwa uchumi wa viwanda hautakuwa na maana yeyote kama bidhaa za ndani hazitapewa kipaumbele.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage katika hafla ya ithibati duniani iliyofanyika katika ofisi za shirika la viwango Tanzania(TBS).
Amesema kuwa Serikali inaendelea na mkakati wake wa kuifanya Tanzania kuwa ya uchumi wa kati unaoongozwa na dira ya maendeleo ya viwanda, hivyo bidhaa za ndani hazina budi kulindwa.
“Viwanda vinaanzishwa kweli kweli, lakini changamoto iliyopo ni namna gani ya kuvilinda viwanda vyetu,”amesema Mwijage.
-
Kubenea asomewa shitaka la kumshambulia mbunge
-
Maaskofu wamkingia kifua JPM, wanena mazito kuhusu mimba mashuleni
-
Serikali yapunguza gharama za umilikaji ardhi
Hata hivyo, Mwijage ameiomba TBS kuvilinda viwanda hivyo kwa kutoruhusu kuingia bidhaa nchini zisizo na ubora ili kupisha uzalishaji wa bidhaa za ndani