Serikali imesema kuwa kuanzia mwaka huu wa fedha itapunguza gharama za malipo ya awali ya thamani ya ardhi iliyopimwa kutoka asilimia 7.5 mpaka asilimia 2.5

Hayo yamesemwa mapema hii leo bungeni mjini Dodoma na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa wakati akitoa hoja ya kuahirisha mkutano wa bunge la 11.

Amesema Serikali itahakikisha kuwa kila kipande cha ardhi ya Tanzania kinapimwa ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015.

 

“Serikali inaendelea kupunguza gharama za umilikaji wa ardhi nchini na katika mwaka wa fedha 2017/2018, imepunguza tozo ya awali ya ardhi iliyopimwa (premium) kutoka asilimia 7.5 ya thamani ya ardhi hadi asilimia 2.5 tu. Natoa wito kwa wananchi kuchangamkia punguzo hili na kujitokeza kupimiwa na kumilikishwa ardhi,” amesema Majaliwa

Hata hivyo, ameongeza kuwa Serikali itaendelea kuimarisha Ofisi za Ardhi za Kanda kwa kupeleka wataalam wa kada mbalimbali na kuwawezesha kwa kuwapatia vitendea kazi stahiki

IGP Sirro apokea msaada wa magari
Mwimbaji wa injili akiri kufanya ujambazi, adai anatafuta pesa atoe albam yake