Rais mstaafu wa awamu ya pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi jana amezungumza katika ibada iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali jijini Dar es salaam na kutoa salamu zake za Eid el Fitr, ambapo amempongeza Rais Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuwatumikia watanzania.
Mwinyi amesema kuwa laiti katiba isingekuwa na kipengele cha ukomo wa madaraka ya Rais, angeshauri Magufuli awe kiongozi wa siku zote.
” kuwa tunakatiba basi hatuna budi kuifuata. Ila kikubwa Watanzania tuzidi kumuombea na kumsaudia Rais wetu,” amesema Mwinyi.
Mwinyi maarufu kama mzee wa Ruksa amesema, Rais Magufuli amefanya kazi kubwa ya kuwaongoza wananchi, hivyo amewaomba wananchi kuendelea kushikamana na kumuunga mkono Rais Magufuli.
”Waswahili wanasema kidole kimoja hakivunji chawa”.
Kwa upande wa Dk.Hussein Mwinyi amewasihi Watanzania kuendelea kudumisha matendo waliyofanya katika mwezi wa Ramadhani na Serikali itazidi kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo mbalimbali ikiwemo Kibiti.