Viongozi wa dini nchini wameombwa kuungana kwa pamoja bila kujali itikadi zao za kimadhehebu na kukemea mauaji yanayoendelea Mkoa wa Pwani katika wilaya za Kibiti na Mkuranga.

Hayo yamesemwa mapema leo na Sheikh Mkuu wa dhehebu la Shia Ithna Shariya, Hemed Jalala katika swala ya Eid iliyoswaliwa katika msikiti wa Al Ghadir uliopo Kigogo, Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

Sheikh Jalala amesema viongozi wa dini wanafursa kubwa ya kuongea na waumini wao na matukio hayo yafikie ukomo kwani yanayoendelea Kibiti yanalitia aibu taifa na siyo utamaduni wa watanzania.

Amesema akili inapowekwa kando katika kufanya maamuzi ya mambo mbalimbali kunahatari kubwa inaweza kulikumba taifa ikiwemo kutokuwepo kwa maamuzi yenye busara na hekima ambayo hupelekea taifa katika vitendo vya kikatili na ugaidi.

Sheikh Jalala amewasihi waislamu wafanye matendo yao kwa kuzingatia akili, kwani kwa kufanya hivyo kutapelekea kutokubaguana kwa dini, kabila na kupelekea kuwa na taifa bora lenye kuhurumiana na kusaidiana.

Video: Waziri Mkuu apiga marufuku usafirishaji chakula nje ya nchi, atoa agizo kali
Binti wa Sassou Nguesso kitanzini kwa rushwa