Mgombea urais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kupitia chama cha mapinduzi CCM, Dkt. Hussein Ally Mwinyi, amerejesha fomu ya kuwania kuteuliwa na tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), kugombea nafasi hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kurejesha fomu katika ofisi za ZEC, Mwinyi amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura tarehe 28 Oktoba.
Akijibu swali la mwandishi wa habari, Mwinyi amekumbushia kuwa kwa mujibu wa sheria za nchi watakaoruhusiwa kupiga kura ni wale tu wanaoishi nchini.
- Dkt Mwinyi kuchukua fomu ya kugombea urais wa Zanzibar leo
- Mwinyi ataja sababu za kugombea urais Zanzibar
Mwinyi alichukua fomu Agosti 26, na amekuwa mgombea wa kwanza Zanzibar kurejesha fomu za kuteuliwa na ZEC, zoezi linalotarajiwa kukamilika Septemba 9.