Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera amewatahadharisha wachezaji wake wapya waliosajiliwa msimu huu kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania bara VPL.

Yanga inatarajia kucheza nyumbani katika Uwanja wa Taifa na Ruvu Shooting, kwenye mchezo wa kwanza wa ligi.

Aidha, kuelekea mchezo huo, kocha Zahera amewataka wachezaji wake wapya kutodharau mechi yoyote, huku akisisitiza kuwa wachezaji wa Kimataifa ambao hawakucheza mechi za Klabu Bingwa Afrika kwa sababu ya vibali, wako fiti kucheza mechi za ligi.

Nimewaambia wachezaji wote wapya kwamba hakuna hata siku moja Yanga inacheza mechi nyepesi, mechi zote ni ngumu, Wachezaji wote ambao hawakupata leseni za kucheza mechi za CAF wote watakuwa na nafasi ya kucheza ligi,”amesema Zahera

Yanga ilirejea usiku wa kuamkia Jumatatu kutoka nchini Botswana ambako ilicheza mechi ya marudiano na Township Rollers na kufanikiwa kuvuka hatua ya pili ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika kwa utofauti wa bao moja.

 

Walioandamana Ubalozi wa Afrika Kusini kudai ndege ya Tanzania iachiwe wakamatwa
Rais wa kwanza wa Gambia afariki dunia