Msanii wa muziki wa bongo fleva Q-Chief amekanusha taarifa inayosema kuwa amehama dini ya uislamu na kuhamia dini ya ukristu madai hayo yamezuka mara baada ya msanii huyo kuonekana karibu na mchungaji Anthony Lusekelo maarufu kama Mzee wa upako.
Japokuwa msani huyo amekiri kuwa karibu na mchungaji Lusekelo na kusema anamchukulia kama kaka yake na anapenda sana ambavyo mchunguji huyo amekuwa karibu katika kumshauri mambo mbalilmbali.
Q-Chief ambaye hivi sasa anafanya vizuri na ngoma yake ya ‘Naogopa’ amesema
-
Diamond kung’arisha upya nyota ya Mr. Nice
-
Times FM kuzindua msimu mpya wa kipindi chake
-
Lulu ataja kinachozimaliza filamu za kitanzania
“Familia yangu upande wa mama wengi ni wakristo, lakini wamegawanyika kutoka kwenye uislam kwenda ukristo, baba yangu ni muislam, babu yangu ana msikiti kwa hiyo sio jambo jepesi kutoka kwenye dini yangu imani yangu kwenda kwenye imani nyingine, naamini Mungu ndiye jibu sahihi, lakini huwa nachukua ushauri wa viongozi wa dini tofauti tofauti”,
Aidha ameongeza kwa kusema “Kuna siku moja nilipigiwa simu usiku kama saa saba hivi, kupokea ni Mzee wa Upako nikashtuka, nikasema kuna kitu gani au zali zimenindondokea! lakini nikagundua ni shabiki yangu namba moja”.
”Na siku zote amekuwa akitamani kunishauri, kunijenga kiimani lakini pia kuzungumza na mimi kama kijana, kwamba lolote unalopitia usisahau Mungu amekuweka kwa sababu, na Mungu yupo kuwainua wale walioanguka, naheshimu ushauri wake kama kiongozi, kama kaka mshauri kama mchungaji”, amesema Q Chief.