Muigizaji Elizabeth ‘Lulu’ Michael amesema kuwa tatizo kubwa linalozamisha tasnia ya uigizaji nchini (Bongo Movies) ni kuiga kilichofanywa na mtu mmoja aliyeonekana kufanikiwa.

Lulu amesema kuwa tabia hiyo huua ubunifu kwa waongozaji na waigizaji wa filamu wakijikuta wanatoa kazi zinazofanana.

“Binafsi naweza kusema kuwa kuna sehemu moja tulikuwa tunaitazamia, unajua kuna kitu kinatokea kama upepo ukiona mtu kafanikiwa kwa kitu fulani wote tunataka kwenda kwenye same direction. ,” Lulu amewaambia waandishi wa habari.

“Kuna mtu mmoja alifanikiwa sehemu mmoja na sisi wote tukawa tunataka kukopi the same direction, so that is a Problem,” ameongeza.

 

Katika hatua nyingine, Lulu ameeleza kuwa filamu yake mpya aliyoitoa hivi karibuni haikufanikiwa sana kutokana na kuiuza kwa njia ya mtandao ambayo haijazoeleka kwa watu wengi.

Alisema kutokana na hali hiyo, wanajifunza upungufu uliojitokeza kwenye mauzo  ya filamu hiyo mtandaoni hivyo watayatumia kuboresha kazi nyingine watakazozitoa na kuziuza kwa njia hiyo.

Times FM kuzindua msimu mpya wa kipindi chake
Makonda apiga ‘stop’ amri ya kuondoa tinted kwenye magari