Kocha Mkuu wa Young Africans Nasreddine Nabi amewatahadharisha wachezaji wake wakiwemo washambuliaji, Kennedy Musonda na Fiston Mayele kwa kuwaambia kuwa bado hajawafuzu Nusu Fainali licha ya kufanikiwa kupata ushindi katika mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa Robo Fainali dhidi ya Rivers United, hivyo wanatakiwa kutumia nafasi za kufunga kwenye mchezo wa Mkondo wa Pili utakaopigwa kesho Jumapili (Aprili 30) ili kufikia lengo la kusonga mbele.

Young Africans imejiwekea mazingira mazuri ya kufuzu Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika baada ya kushinda 2-0 dhidi ya Rivers, katika mchezo wa Mkondo wa Kwanza uliopigwa Jumapili (Aprili 23).

Akiwa katika maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo huo Kocha huyo kutoka nchini Tunisia amesema: “Hatuna presha kwa sababu tumefanikiwa kupata matokeo katika mchezo wa kwanza, ingawa bado tuna kazi kubwa ya kufanya kuhakikisha tunaendelea kupata matokeo katika mchezo ambao tutacheza nyumbani kwa sababu wapinzani wana timu yenye wachezaji wazuri ambao wanaweza kufanya mambo kuwa tofauti.”

“Lakini sitaki kuona tunawadharau kwa kuwa tumefanikiwa kupata matokeo ya awali, hatua ambayo tupo kwa sasa inahitaji kuweka nguvu na kila mmoja kutoa mchango wake ili kuweza kupata matokeo kwa kutumia kila nafasi ambayo itakayoweza kupatikana kwa sababu watahitaji kupata matokeo mazuri kwetu hivyo lazima tuwe bora zaidi yao,”

COSTECH yaiasa jamii kusaidia, kuwekeza kwenye ubunifu
Nelson Okwa mambo magumu Ihefu FC