Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Nasreddine Nabi, amewasihi viungo wake kwa kuwataka kuwa makini watakapocheza ugenini dhidi ya Rivers United ya Nigeria mwishoni mwa juma hili.

Young Africans inayotarajiwa kuondoka kesho Alhamis (April 20), itakabiliwa na mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa Robo Fainali Kombe la Shirikisho Barani Afrika katika Uwanja wa Kimataifa wa Godswill Akpabio, Uyo nchini Nigeria.

Kocha Nabi amesema Wachezaji wake hawatakiwi kurudia makosa waliyoyafanya katika mchezo uliopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Simba SC, ili kurejesha muendelezo wa kupata matokeo mazuri, na kuwafurahisha Mashabiki na Wanachama wao.

“Katikati tulionekana tupo pungufu kutokana kutokuwa makini kutocheza mpangilio, tunahitaji mmoja ushindi tunakokwenda, kila naomba atambue majukumu yake,” amesema.

Kocha huyo amesema kikosi chake kitaingia katika mchezo dhidi ya Rivers United kwa tahadhari kwani wanahitaji kushinda ili wakae katika nafasi nzuri ya kutinga Nusu Fainali.

Young Africans ilitinga Robo Fainali baada ya kuwa kinara wa Kundi D ikiwa na alama 13 sawa na US Monastir ya Tunisia iliyomaliza nafasi ya pili kwa utofauti wa mabao ya kufunga.

AS Real Bamako ya Mali ilishika nafasi ya tatu ikiwa na alama tano wakati TP Mazembe ya DR Congo ikiburuza mkia kwa kuwa na alama tatu.

Mkutano wa Azimio la Umoja waahirishwa
Sambou kuikosa Simba SC Jumamosi