Kocha Mkuu wa Young Africans Nasreddine Nabi, anaamini umahiri wa Mlinda Lango wa Simba SC Aishi Manula ulikua kikwazo kwa kikosi chake kupata ushindi Jumamosi (Desemba 11).

Young Africans walialikwa na Simba SC waliokua Wenyeji wa mchezo huo, Uwanja wa Benjamin Mkapa na mwisho wa dakika 90 timu hizo zilishindwa kufungana.

Kocha Nabi amesema kuwa isingekuwa ni Manula basi wangeifunga Simba SC kwenye mchezo huo kwa kuwa walitengeneza nafasi nyingi ambazo zilikuwa zinawapa uhakika wa ushindi.

“Yule kipa wao (Aishi Manula) amefanya kazi kubwa kwenye kuokoa mipira yetu, kwa mfano kuna mpira ulipigwa na Said Ntibanzokiza unadhani asingekuwa imara nini kingetoa zaidi ya kuwa bao?” amehoji Kocha Nabi

“Itoshe kusema kwamba ni kipa mzuri na ukitengemea kwamba ni kipa ambaye anadaka kwenye timu ya taifa, (Taifa Stars). Ni mambo ya mpira huwa yanatokea lakini ninaweza kusema kwamba wachezaji wangu walicheza vizuri,” amesema Kocha Nabi.

Manula anafikisha jumla ya michezo minane kukaa langoni huku akiwa ameruhusu kufungwa mechi mbili mabao mawili na kwenye michezo sita alikuwa shujaa kwa kuwa hakufungwa.

Balozi Kairuki ateta na wanafunzi mjini Wuhan China
Simba SC waitikia ombi la Mwekezaji