Nabii Tito aliyejipatia umaarufu baada ya habari zake kusambaa katika mitandao ya kijamii akionekana kufanya ibada kinyume na maadili ya dini huku akitumia biblia kuhamasisha mambo kinyume na dini.
Kupitia matukio hayo, Jeshi la polisi lililazimika kumpeleka Hospitali ya Magonjwa ya Akili, Milembe ambapo ripoti imeonesha kuwa ana matatizo ya akili.
Nabii Tito ameibua mengine baada ya kujijeruhi kwa kujikata na wembe tumboni ambapo kumepelekea ashonwe nyuzi 25 katika zahanati ya polisi Dodoma.
-
Video: Lissu atuma waraka mzito kwa Ndugai, Kigwangalla kushtaki Jeshi la Polisi kwa JPM
-
Daktari atoa ripoti ya ukichaa wa ‘nabii Tito’
-
Video: Tundu Lissu nimetolewa risasi nyingine mwilini, Wabunge 11 wasota kizimbani
Daktari wa hospitali hiyo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na ameeleza kuwa Tito alifikishwa hospitali saa 9 mchana akiwa anavuja damu eneo la tumbo.
”Ni kweli Tito alifikishwa hapa majira ya saa 9 mchana, tulimfanyia matibabu kwa kumshona nyuzi 25 kutokana na ukubwa wa majeraha hayo” amesema Daktari.
Hata hivyo kamanda wa polisi Dodoma, Gilles Muroto hana taarifa kutokea kwa tukio hilo.
Nabii Tito sasa anashikiliwa na polisi kutokana na kauli zake zinazopingana na dini, amekuwa akihamasisha watu kunywa pombe, na wanaume kulala na wadada wa kazi akidai kuwa kufanya hivyo sio dhambi.
Hivyo baada ya matibabu hayo nabii Tito alirudishwa polisi kwa mahojianao zaidi.