Tajiri na Mfanyabiashara mkubwa duniani, Bill Gates amemuonya rais wa Marekani Donald Trump kwa misimamo ya sera yake ya “Marekani Kwanza” kuwa inaweza kuharibu uhusiano wa nchi hiyo na bara la Afrika.

Ameyasema hayo katika mkutano wa dunia wa uchumi World Economic Forum (WEF) unaofanyika huko Davos nchini Switzerland ambapo amesema kuwa kunatakiwa kuwepo kwa uwiano wa wenye nguvu kubwa na nguvu kidogo.

Amesema kuwa Marekani inaweza kupoteza ushawishi wake barani Afrika huku nchi kama China zinazidi kuimarisha uhusiano na bara hilo kwa kuwekeza katika sekta mbalimbali.

Aidha, Bill Gates anamfuko wake barani Afrika unaoitwa Bill & Melinda Gates Foundation, ambao umekuwa ukijihusisha kwa kiasi kikubwa kutoa huduma za afya katika nchi kadhaa.

Hata hivyo, Rais Trump amesema kuwa atakata msaada wa bajeti ya afya kwa takribani dola bilioni 2.2 katika mfuko wa dunia, huku akiwakasirisha viongozi wa Afrika bada ya kuyaita mataifa ya Afrika machafu kupindukia.

Mjema azindua kampeni ya Tumkumbuke na mtoto wa kiume
Nabii Tito aibua mapya, akimbizwa hospitali