Mkuu wa Wilaya Ilala, Sophia Mjema amewataka watoto wa kiume kuwaripoti watu wanaowalazimisha    kufungua zipu za kaptula zao ili wawachungulie maumbile yao.

Amewataka watoto wa kiume kujiamini na kutowaogopa watu wanaotishia au wanaowafanyia vitendo vya ukatili hasa ulawiti hata wakiwatishia kuwaua.

Mjema ametoa wito huo kwa watoto wa kiume Dar es salaam katika shule ya msingi Muhimbili wakati alipokuwa akizindia kampeni ya ”Tumkumbuke na mtoto wa kiume”.

Ambapo kampeni hiyo imelenga kuelimisha jamii kuwalinda watoto wa kiume dhidi ya vitendo vya ulawiti na unyanyasaji unaofanywa kwa woto wa kiume ndani ya jamii.

Aidha Mjema amewaomba watoto wa kiume kutoa taarifa mara moja kwa wazazi wao mara tu wanapokutana na watu wa aina hiyo, ili kuwachukulia hatua na kukomesha tabia hiyo iliyozuka hapa nchini.

Hata hivyoa ameziagiza mamlaka husika kusikiliza, kukusanya ushahidi na kutolea hukumu kesi zinazohusu masuala ya ukatili wa kijinsia, ulawiti na ubakaji.

Ameongezea kuwa Serikali imepoke ombi la wakili wa kujitegemea, Jebra Kambola ameomba kutengeneza sheria kali itayohusu kuwalinda watoto wa kiumbe dhidi ya vitendo vya ukatili wa jinsia hasa ulawiti.

Wasiwasi watanda Raila akijiandaa kuapishwa
Bill Gates atofautiana na Trump kuhusu Afrika