Jeshi la Polisi jijini Nairobi limetandwa na wasiwasi mkubwa baada ya chama cha Nasa kusisitiza na kuapa kuendelea na mipango yao ya kumuapisha Raila Odinga katika Uwanja wa Uhuru.

Ofisa Mkuu Mtendaji wa chama cha Nasa Norman Magaya, amesisitiza hayo jana na kusema kuwa shughuli ya kiapo itaendelea katika uwanja huo kama ambavyo imepangwa.

Mgaya amehojiwa na vyombo vya habari mbalimbali jijini Nairobi amesema kuwa Nasa imetuma maombi kwa Serikali kaunti ya Nairobi kutaka kutumia uwanja huo na walipaswa kuulipia siku ya jana.

Hata hivyo Mgaya amemlalamikia Gavana Mike Sonko kwa hatua  aliyoichukua ya kuufungia ukumbi huo

Aidha Mgaya amewashauri wafuasi wa Nasa kukaidi marufuku hiyo ya kutumia uwanja huo na amewasihi kujitokeza kwa wingi siku hiyo ya uapisho wa Raila Odinga utakaoanza rasmi saa mbili asubuhi.

Milioni 20 zatumika kununua miche ya miti
Mjema azindua kampeni ya Tumkumbuke na mtoto wa kiume