Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Revocatus Kuuli amesema kuwa Jumla ya shilingi milioni 20 zimetuma katika kampeni ya upandaji miti katika maeneo mbalimbali wilayani humo.

Ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti kwa wanachuo wa Chuo cha Sayansi za Afya Nkinga uliofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora

Amesema fedha hizo zimetumika katika ununuzi wa miche ya miti, uoteshaji wa miche na zoezi zima la upandaji katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kurudisha uoto wa asili.

Aidha, ameongeza kuwa kutokana na zoezi hilo kutumia fedha za Halmashauri hiyo zinazotokana na vyanzo vyake wataendelea kupambana na watu wote wanaoendesha uharibifu katika misitu, vyanzo vya maji na wanachunga mifugo katika maeneo ambayo hayaruhusiwi kisheria ili kuhakikisha matunda ya fedha hizo yanaonekana.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amesema kuwa kundi hilo la wasomi ni kundi muhimu sana katika kampeni zinazoendelea Mkoani humo.

Hata hivyo, ameongeza kuwa kundi hilo haliwezi kubaki kuwa watazamaji katika zoezi la upandaji miti linapaswa kuwa sehemu ya mradi huo unaoendelea maeneo mbalimbali mkoani humo ili nao wabakize alama kama waliwahi kukaa na kupata elimu na hatimaye kushirikia katika utunzaji mazingira.

 

Mbowe, Lowassa kumnadi Salum Mwalimu kesho
Wasiwasi watanda Raila akijiandaa kuapishwa