Roma Mkatoliki ni jina liloamka ndani ya fikra za Watanzania baada ya kusikika ngoma ya ‘Tanzania’ iliyokuwa kiharakati, lakini Nahreel ametufungua macho zaidi kuwa yeye ndiye chanzo cha wimbo huo.

Roma Mkatoliki

Roma Mkatoliki

Akifunguka kupitia TV1, Nahreel ambaye ni msanii na mtayarishaji wa muziki na mmiliki wa ‘The Industry’ amesema kuwa yeye ndiye aliyeutengeneza mdundo wa wimbo huo uliomtoa Roma lakini hadi wimbo unatoka na Roma anaanza kuwa ‘nyota’ hakuwahi kumuona.

“Mimi nimetengeneza nyimbo za watu wengi bure, hata wimbo wa Roma ule ‘Tanzania’ uliomtambulisha mimi niliyetengeneza ‘beat’ nikamuachia hata bila kumuona sura,” alisema Nahareel. “Nilikuja kuusikia tu wimbo umetoka,” aliongeza.

‘Tanzania’ ni moja kati ya nyimbo zilizomtambulisha Roma kama msanii wa Siasa (Politician MC) na kumpa mashabiki wengi lakini baadae alizoa mashabiki wengi zaidi baada ya kuanza kutoa nyimbo nyingine kali zisizohusu siasa akiwa chini ya Tongwe Records.

Majaliwa aongoza Wananchi kuaga miili ya waliokufa tetemeko la ardhi, Atoa agizo TMA
Diwani apigana ngumi na Mwenyekiti kumgombea Ofisa Mtendaji