Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi amemwagiza Meneja wa Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Babati Mhandisi Felix Mollel, kumuondoa haraka fundi wa miundombinu ya maji anayesimamia mradi wa maji Katika kijiji cha Gidas wilayani Babati, Amos Abi.


NAibu Waziri Mahundi amechukua uamuzi huo baada ya kubaini baadhi ya vituo vya kuchotea maji kijijini hapo havitoi huduma kutokana na fundi kutovifanyia matengenezo licha ya kupewa vitendea kazi vyote.

Aidha, ametoa siku tano kwa Meneja wa RUWASA wilayani humo kuhakikisha kasoro zote zilizobainika zinatatuliwa na maeneo yote yanapata maji.

Vile vile amewataka wataalam wa maji kote nchini waachane na tabia yakukaa ofisini bali watembelee miradi yao ili kubaini changamoto kwa haraka.

Naibu Waziri wa Maji MaryPrisca Mahundi yuko mkoani Manyara kwa ziara ya kikazi.

Pichani ni Fundi Amos Abi, upande wa (kushoto) akijieleza mbele ya Naibu Waziri wa Maji Muhandisi Maryprisca Mahundi wakati wa ukaguzi wa mradi huo mkoani MAnyara Wilaya ya Babati
Meneja RUWASA Babati Eng. Fellix Molel akipokea maelekezo kutoka kwa Naibu Waziri wa Maji Maryprisca Mahundi wakati wa ukaguzi wa mradi wa maji Katika kijiji cha Gidas wilayani Babati

Chui amjeruhi mwanamitindo
Akutwa akifanya tendo la ndoa na mwanafunzi wa darasa la nne