Mwanamitindo aliyejulikana kwa jina la Leidolph (36) ameshambuliwa na chui baada ya kupiga picha katika makazi ya wastaafu yaliyotengwa kwa ajili ya maonyesho ya wanyama Mashariki mwa Ujerumani.

Kwa mujibu wa Gazeti la Bild nchini humo limeeleza kuwa mwanamitindo huyo aliyependa wanyama na mitindo alijeruhiwa vibaya kichwani na chui wawili ambao wapo ndani ya hifadhi hiyo wanaojulikana kama Troy na Paris.

Hata hivyo Jeshi la Polisi nchini humo limethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo wamesema kuwa mwanamitindo huyo alifikishwa hospitali akiwa na majeraha katika mwili wake.

Mamlala katika eneo la Burgenland zimesema hakuna hatari yoyote kwa wakazi na kuongeza kuwa uchunguzi unaendelea kubaini kilichotokea katika mkasa huo wa Nebra katika jimbo la Saxony-Anhalt.

Waitara atoa maagizo kwa taasisi za miundombinu
Naibu Mahundi aagiza Fundi msimamizi wa mradi wa maji Babati kuondolewa