Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk amesema mashindano ya baiskeli yana umuhimu mkubwa ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na zaidi yanafanya ushirikiano wa nchi wanachama kuendelea kuhimarika.
Ameyasema hayo leo katika uzinduzi wa safari kwa waendesha baiskeli 42 ambao wameanza safari hapa nchini na kutembelea nchi mwanachama wa Afrika Mashariki kwaajili ya kuhamasisha ushirikiano ndani ya jumuiya hiyo inayoundwa na nchi za Tanzania,Kenya,Uganda, Burundi na Rwanda.
katika safari hiyo watatumia zaidi ya kilomita 6000 kupitia katika miji mikuu ya nchi hizo na baadae watamalizia mmkoani Arusha.
Akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa mashindano hayo ya nne yanayotambulika kama ‘Great African Cycling Safari’ Mhe.Mbarouk amesema mashindano hayo yatakayokwenda katika miji ya Nairobi, Kampala, Kigali, Bujumbura, Dodoma na kuishia Jijini Arusha, yana kila sababu ya kuungwa mkono na wana Afrika Mashariki wote kwa kuwa yatazitangaza nchi Jumuiya katika mataifa mbambali wakati waendesha baiskeli hao watakapokuwa wakipita.
“Hii ni alama kubwa ya ushirikiano kwa nchi za Afrika Mashariki na zaidi yanahimarisha ushirikiano wetu, sisi kama viongozi wa Jumuiya tunaona kwa namna gani ya kuishauri Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuyaweka mashindano haya katika kalenda yake ili pamoja na mambo mengine yawe katika utaratibu unaotambulika” amesema Mbarouk.
Kwa upande Balozi wa Kenya hapa nchini Mhe. Dan Kazungu, amesema mashindano hayo yatakayotazamwa na mamilioni ya watu Duniani kote yatasaidia kutangaza vivutio mbalimbali vilivyopo katika nchi za Afrika Mashariki sambamba na kuwavutia watu wengi zaidi kuja na kushiki mashindano hayo.
Amesema mashindano ‘Great African Cycling Safari’ yanayohusisha umbali wa Kilomita 6000 yakitumia siku 55, yana mvuto zaidi ya yale yanayojulikana kama ‘France De Tour’ ya nchini Ufaransa ambayo huusisha umbali wa Kilomita 3000 huku yakitumia siku 12 za mashindano.
Aidha Mhe.Kazungu amewataka wananchi wote ambapo waendesha baiskeli hao watapita kushiriki kwa kuendesha kuwashangilia na kuwatia moyo ili kuwapa hamasa waendeshaji hao aliowaita ‘mashujaa’ waliojitolea kuitangaza Afrika Mashariki.
“Niwasihi waendesha baiskeli wote mnaoshiriki katika mashindano haya kutimiza malengo ya mashindano yaliyokusudiwa na waandaaji licha ya uwepo wa changamoto mbalimbali mnazoweza kukutana nazo” amesema Kazungu.
Amesema mashindano hayo yanaonyesha alama kubwa ya ushirikiano ndani ya jumuiya na zaidi akasisitiza yaendelee kutangazwa kwa ajili ya kuwavutia watu wengi zaidi kuja kushiriki hatua ambayo pamoja na mambo mengine kutaiwezesha jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa imara,
Naye Mkurugenzi wa ‘Great African Cycling Safari’ Bw.John Balongo amesema mashindano hayo yaliyoanzishwa Mwaka 2016 yakishirikisha watu saba, yanazidi kupata chachu siku hadi siku hadi mwaka huu yanaposhirikisha watu 42 kutoka mataifa yote ya Afrika Mashariki.
Amesema kilichosababisha idadi ya washiriki kuendelea kuongezeka ni hamasa iliyopo pamoja na uzalendo wa washiriki wote na kusisitiza kuwa dhamira yao kuyafanya mashindano hayo kuwa namba moja kwa ubora duniani.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (kulia mwenye suti) akiwatazama waendesha baiskeli katika ufunguzi wa safari ya Waendesha Baiskeli 42 kutoka nchi sita za Afrika Mashariki yanayotambilika kama ‘Great African Cycling Safari’ .Uzinduzi huo umefanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akizungumza katika ufunguzi wa mashindano ya safari ya Waendesha Baiskeli 42 kutoka nchi sita za Afrika Mashariki yanayotambulika kama ‘Great African Cycling Safari’ .Uzinduzi huo umefanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Kenya hapa nchini Mhe. Dan Kazungu akizungumza katika ufunguzi wa mashindano ya safari ya Waendesha Baiskeli 42 kutoka nchi sita za Afrika Mashariki yanayotambulika kama ‘Great African Cycling Safari’ .Uzinduzi huo umefanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa ‘Great African Cycling Safari’ Bw.John Balongo akizungumza katika ufunguzi wa mashindano ya safari ya Waendesha Baiskeli 42 kutoka nchi sita za Afrika Mashariki yanayotambulika kama ‘Great African Cycling Safari’ .Uzinduzi huo umefanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (katikati) akiwa katika mazungumzo na upande Balozi wa Kenya hapa nchini Mhe. Dan Kazungu (kulia) pamoja na Naibu Balozi wa Uganda nchini Tanzania katika uzinduzi rasmi wa mashindano ya baiskeli ya nne yanayotambiulika kama ‘Great African Cycling Safari’ .
Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini Chama Cha Baiskeli Tanzania (CHABATA) akizungumza katika ufunguzi wa mashindano ya safari ya Waendesha Baiskeli 42 kutoka nchi sita za Afrika Mashariki yanayotambulika kama ‘Great African Cycling Safari’ .Uzinduzi huo umefanyika leo Jijini Dar es Salaam.