Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema anaipongeza kampuni ya BHATI AIRTEL kwa kuwa wazalendo kwa kuweza kulipa Gawio la shilingi bilioni tatu.
Ameyasema hayo Ikulu jijini Dar es salaam alipokuwa akiwaapisha viongozi na kupokea gawio kutoka kampuni ya BHATI AIRTEL, ambapo amesema kuwa kampuni hiyo imeonyesha uzalendo wa hali ya juu.
Ameihakikishia kampuni hiyo uwezekezaji wenye uhakika na salama, hivyo ameyataka makampuni mengine kama VODACOM, TIGO, ZANTEL na HALOTEL kuiga mfano wa kampuni hiyo ya BHATI AIRTEL.
”Nawashukuru na kuwapongeza kwa upande wa serikali na BHATI AIRTEL kwa wale wote walioshiriki katika majadiliano haya, yamechukua muda mrefu lakini mmefanikisha mpaka BHATI AIRTEL wamelipa,”amesema Rais Magufuli
Hata hivyo, Rais Magufuli ameitaka kampuni ya BHATI AIRTEL, kukamilisha leo leo kiasi kidogo kilichobaki kabla ya mkurugenzi huyo kuondoka nchini kuelekea India.
-
JPM: Nilikuwa nimejiandaa kuifuta kampuni ya Airtel
-
LIVE IKULU: Rais Magufuli akiwaapisha viongozi na kupokea Gawio kutoka kampuni ya BHATI AIRTEL
-
Video: Mawaziri 7 ambao hawajaguswa na JPM, Utata wagubika kifo kigogo wa polisi