Uongozi wa Namungo FC umetoa ufafanuzi wa kuendelea kumtumia kiungo mshambuliaji Shiza Ramadhan Kichuya kwenye michezo ya Ligi Kuu na michuano ya kimataifa, licha ta taarifa kutoka FIFA kueleza mchezaji huyoa mefungiwa kwa miezi sita.
Kichuya alisajiliwa na Simba kwenye usajili wa Januari akitokea Klabu ya Pharco ya Misri ambayo inadai kuwa alikuwa na mkataba wa miaka miwili na alitumia mkataba wa mwaka mmoja, jambo lililowafanya wapeleke malalamiko hayo kwa FIFA kulalamikia suala la usajili wa mchezaji huyo.
Hatua hiyo imeilazimu FIFA kutangaza kumuadhibu Kichuya kwa kumfungia kucheza soka kwa miezi sita, huku Simba FC wakitozwa faini ya zaidi ya shilingi milioni 250.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mwasilino Namungo FC Kindamba Namlia amesema, Kichuya ataendelea kutumiwa na klabu hiyo kwa sababu Klabu ya Simba imeomba FIFA kufanya mapitio upya ya shauri linalomhusu mchezaji huyo.
“Katika taarifa tuliyopewa kuhusu Kichuya inasema, Kichuya anaweza kufungiwa miezi sita endapo Klabu ya Simba itashindwa kulipa faini ndani ya siku 45.”
“Mshtakiwa namba moja kwenye shauri lile Shiza Kichuya anaweza kufungiwa miezi 6, mshtakiwa namba mbili Simba SC inaweza kufungiwa kusajili kwa misimu mitatu (madirisha matatu makubwa ya usajili).”
“Kwa sasa Simba imeomba mapitio ya hukumu iliyotolewa na FIFA, kwa maana hiyo kila kitu kinaanza upya hadi mapitio yatakapokamilika. Maana yake hata ule muda iliopewa Simba kulipa faini hauangaliwi hadi pale mapitio yatakapokamilika.”
“Taarifa itakayotoka baada ya mapitio ndio itafanya kazi.Sisi tunajitahidi kwenda kiwekedi, baada ya kuipata taarifa kuhusu Kichuya mtu wetu wa sheria hakuwepo kwa hiyo tulisubiri hadi asome nyaraka za taarifa tuliyopewa kuhusu Kichuya na atupe tafsiri yake.”
Hata hvgo tangu taarifa za FIFA zilipotolewa na kuripotiwa na vyombo vya habari nchini, Namungo FC hawajamtumia Shiza kichuya kwenye michezo ya Ligi Kuu dhidi ya Biashara United Mara na kisha Azam FC.