Mrembo wa video za muziki na filamu Tanzania , Nana amefunguka ugumu anaopitia katika sanaa yake ya kuigiza .
Akizungumza mbele ya Kamera ya Dar 24, Nana amesema kuwa anapata shida sana kuigiza kipande cha mapenzi katika kazi yoyote anayopata , kwani anajisikia huru kufanya hivyo na mume wake pekee.
“Napata ugumu kuigiza scene ya kuwa romantic kwasababu sijawahi kufanya hivyo na mwanaume mwingine yeyote tofauti na mpenzi wangu , inakuwa ngumu sio rahisi ‘kukisi’ unajua eeh, au kuigiza kulia sio kitu rahisi,” alisema mrembo huyo .
Nana amesema kuwa mbali na kutopenda kuigiza mambo ya mapenzi, anafurahia sana kufanya kazi kwa ratiba na ushirikiano toka kwa wasanii wenzake .
Angalia mahojiano kwa kina hapa: