Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye, amewataka wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kufanya kazi kwa ari ili kuhakikisha linakuwa mfano Barani Afrika katika kuhabarisha umma.
Nape ameyasema hayo mapema hii leo alipofanya ziara katika Shirika hilo ili kuona utendaji kazi pamoja na kuona changamoto mbalimbali zinazolikabili Shirika hilo.
“Fanyeni kazi kwa bidii na uadilifu kwa kutoa taarifa za ukweli na zenye uhakika kwa watazamaji puuzeni propaganda zinazoenezwa mtaani kuwa Shirika hili limepoteza Watazamaji na wasikilizaji kwa manufaa ya Taifa letu”.Amesema Waziri Nape.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Dkt.Ayoub Ryoba amesema kuwa Shirika linaendelea kuongeza wasikilizaji na watazamaji ambapo kuanzia mwaka 2012 hadi 2016 limeongeza mitambo kutoka kumi na mbili hadi hadi kumi na tisa iliyofungwa Mtwara,Rombo,Mbambabei na Tarime.
Aidha, Dkt Ryoba ameongeza kuwa Shirika hilo bado linaendelea kuwa katika historia ya Kuwa Shirika lililohabarisha umma juu ya Jitihada za Serikali ya Tanzania katika Ukombozi wa Bara la Afrika pamoja na kuendelea kukuza lugha ya Kiswahili kupitia kipindi cha malenga wapya.
“Shirika letu linaendelea kutoa habari, elimu na burudani zinazozingatia muktadha wa Utamaduni wa Nchi yetu ambapo kwa kipindi cha mwaka jana tumekuwa tukirusha matukio mubashara kupitia mitandao ambayo yana wafuatiliaji zaidi ya million tano.” Alisema Dkt.Ryoba.
Shirika hilo linaendelea kuwafikia watazamaji na wasikilizaji wengi zaidi ndani na nje ya nchi kwa kuendelea kuweka mikakati ya kuongeza vituo vingi zaidi