Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye, amesema kuwa viongozi wa vyama vya siasa kwa hoja moja ya kuunga mkono jitihada za Rais Dkt. Magufuli linampa ukakasi.
Amesema kuwa kuna haja ya kupitiwa upya kwa sheria inayosimamia thamani ya kura hasa katika kipindi hiki cha wabunge na madiwani kuhama vyama vyao.
Aidha, amesema kuwa ni vyema kukawa na sheria ambayo itampa mamlaka mbunge au diwani anayehama chama baada ya uchaguzi, aendelee kuwa na nafasi hizo katika chama anachokwenda ili kuokoa kiasi kikubwa cha fedha kinachotumika katika chaguzi ndogo kwenye maeneo ambayo mbunge au diwani amehamia chama kingine.
“Siwezi kupingana na Katiba kuhusu hamahama za wanasiasa lakini ni vyema thamani ya wapiga kura ikatambulika vyema, bado thamani ya mpiga kura inapaswa kuenziwa,”amesema Nape
-
Nape ataka watungiwe sheria kali wanaohama vyama
-
Madiwani wanne wa Chadema wasimamishwa
-
Chadema yateua watakao gombea, Ukonga,Korogwe na Monduli
Hata hivyo, ameongeza kuwa pamoja na uwepo wa wimbi kubwa la wanasiasa kuhama, wapigakura wanatakiwa kupewa thamani yao kwa kuwa wakati wa uchaguzi wao ndio walihitajika kupiga kura kuchagua wawakilishi wao.