Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Young Africans Nasreddine Nabi amewasili salama Afrika Kusini, tayari kwa kukamilisha taratibu za kusani mkataba na Klabu ya Kaizer Chiefs.
Nabi amewasili nchini humo, akitokea Tanzania ambako amefanya kazi kwa miaka mitatu akiwa na Young Africans huku akipata mafanikio makubwa katika misimu miwili iliyopita kwa kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho mara mbili mfululizo.
Baada ya kuwasili mjini Johannesburg, Kocha huyo alihojiwa na baadhi ya Wanahabari kuhusu matarajio yake ndani ya Kaizer Chiefs, lakini alichowajibu kimeleta mshangao mkubwa.
Kocha Nabi amesema: Natarajia ushirikiano mkubwa kutoka kwa viongozi wa klabu yangu mpya, lakini ifahamike kuwa mimi sio Kocha mkubwa, lakini ninaipenda kazi yangu.
Wakati Kocha Nabi akitoa kauli hiyo baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Rand Soweto, ambao upo eneo yalipo makazi ya Amakhosi [Kaizer chiefs], upande wa Shabiki wa Young Africans anayeitwa Mvano Sports yeye amepost katika mitandao ya kijamii kw kwa kuweka picha ya Aliyewahi kuwa Kocha Mkuu wa Al Ahly ya Misri, Mamelodi Sundowns na Timu ya taifa ya Afrika Kusini Pisto Mosimane akiwa na Mfadhili na Mdhamimi wa klabu hiyo Ghalib Said Mohamed.
Picha ya wawili hao imenakshiwa kwa maneno yanayosomeka: chuma hunoa chuma.
Usiku wa kuamkia leo Young Aficans ilithibitisha kuondoka kwa Kocha Nabi kwa kutoa taarifa rasmi iliyowekwa katika Mitandao ya Kijamii ya Klabu hiyo.