Serikali ya Marekani inatarajia kutangaza katazo pana zaidi la nchi takribani 6 kupata viza za kuingia nchini humo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Uingereza, Reuters, Marekani itasitisha kutazo la viza ambazo zinaweza kupelekea mtu kupata ukazi wa kudumu Marekani.

Ametaja nchi hizo kuwa ni Eriteria, Kyrgyzstan, Myanmar, Nigeria, Tanzania na Sudan ambapo kwa Tanzania na Sudan Serikali ya Marekani itaacha kutoa “visa zinazotolewa kwa mataifa tofauti” visa inayoenda kwa jina la viza ya bahati na sibu inayopatikana kwa waombaji wa nchi zenye idadi ndogo ya wahamiaji walioko Marekani.

Nchi hizo sita zimeshindwa kukidhi viwango vya kubadilishana taarifa na masuala ya kiusalama, iliyopelekea umuhimu wa katazo hili jipya.

Kaimu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Marekani, Chad Wolf, amesema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari Ijumaa.

Matatizo yaliyoelezwa na Wolf ni kati ya teknolojia inayotumika ya pasipoti za kusafiria na kushindwa kwa nchi hizo kubadilishana taarifa juu ya washukiwa wa ugaidi na wahalifu.

Pia ameeleza kuwa Viza za uhamiaji zinazokusudiwa kusitishwa ni tofauti na zile zisizo kuwa za uhamiaji ambazo zinatolewa kwa wanaofanya ziara Marekani, ambazo hazitoathiriwa na katazo hili, Wolf amesema.

Katazo la awali la kusafiri – lililotolewa wakati Trump yuko katika wiki yake ya kwanza madarakani Januari 2017 – lilikuwa ni katazo lililohusisha takriban wahamiaji wote na wasafiri kutoka nchi saba zenye Waislamu waliowengi.

Sera hiyo ilirekebishwa wakati mahakama ikiipinga, lakini Mahakama ya Juu ya Marekani hatimaye iliwafiki na kuipitisha Juni 2018.

Katazo hilo lilioko linahusisha nchi zenye Waislamu waliowengi ambazo ni Iran, Libya Somalia, Syria and Yemen. North Korea na Venezuela ambazo zinakabiliwa na katazo la viza, lakini hatua hizo huwaathiri wasafiri wachache ukilinganisha na wale wanaoruhusiwa kuingia Marekani.

Kevin-Prince Boateng aweka rekodi ya kipekee, atimkia Uturuki
Ally Mayai Tembele: Yanga inajidanganya yenyewe