Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wameridhia rasmi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kujiunga kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Kutokana na uamuzi huo, EAC kwa sasa inafikisha wanachama saba ikiwemo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Sudan Kusini na DRC yenyewe.

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ambaye alikuwa mwenyekiti wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za EAC wa 19 wa Kawaida mbao umefanyika kwa njia ya mtandao wa Zoom leo Machi 29,2022 amesema kuwa,DRC kukubaliwa kuingia EAC kunaashiria tukio muhimu katika historia ya ushirikiano wa jumuiya hiyo.
DRC inapoingia EAC inafanya eneo la jumuiya hiyo kuwa na watu zaidi ya milioni 280 na uchumi wenye pato halisi (GDP) ya dola bilioni 262.
Wakati akihutubia mkutano huo wa Wakuu wa Nchi EAC, Rais Kenyatta ambaye ndiye mwenyekiti amesema kuwa, ujio wa DR Congo katika jumuiya hiyo kutaiwezesha kupata maendeleo yanayohitajika kwa kuzingatia uchumi wa nchi kwa kiasi kikubwa.

Kamati ya Bunge yapitisha makadirio ya mapato na matumizi wizara ya madini mwaka wa fedha 2022/23
Makamu wa Rais kuzindua mbio za mwenge April 2