Kocha Mkuu wa Azam FC, Etiene Ndayiragije, amesema kuwa mpango wao kwa sasa ni kuwafuatilia kwa umakini wapinzani wao kwenye kombe la shirikisho barani Afrika wa kimataifa ambao ni timu ya Triangel FC kutoka Zimbabwe .
Ndayiragije amesema kuwa hadi sasa tayari ameona makosa yaliyopo kwenye kikosi chake na ameanza kuwapa mafunzo maalumu vijana wake kwaajili ya mchezo wao wa kimataifa.
“Nimegundua makosa ya vijana wangu na uwezo wao pia, taratibu ninakuwa na kikosi bora ambacho kitahimili mikikimikiki ya kimataifa nina imani ya kupata matokeo chanya.
“Kwa kuwa tutakuwa nyumbani ni wakati wa mashabiki kuendelea kutupa sapoti kama ambavyo walifanya awali kwenye mchezo wetu dhidi ya Fasil Kenema,” amesema Ndayiragije.
Triangele imefuzu hatua ya awali ya michuano ya Kombe la Shirikisho baada ya kuiondosha Rukizno ya Burundi kwa jumla ya mabao 5-0 ambapo wanatarajiwa kuchuana na Azam FC iliyoiondosha Fasil Kenema ya Ethiopia kwa jumla ya mabao 3-2, kati ya Septemba 13 -15.