Vyombo vya usalama nchini Sudan vimesema shambulizi la Ndege Nyuki kwenye soko la wazi kusini mwa mji Mkuu wa nchi hiyo Khratoum, limeua takriban watu 43, wakati jeshi la Serikali na kundi la wanamgambo wa RSF walopokuwa wakiendeleza mapambano ya udhibiti wa Taifa hilo.

Taarifa juu ya tukio hilo zimeeleza kuwa, watu wengine 55 wamejeruhiwa katika shambulizi hilo kwenye kitongoji cha May, ambako wapiganaji wengi wa RSF walikuwa wakitekeleza mashambilizi kadhaa ambayo yameleta athari kwa jamii isiyo na hatia.

Kundi la Wanaharakati la Resistance Committee ambalo hupanga misaada ya kibinadamu limeweka video kwenye mitandao ya kijamii, ikionyesha miili ya watu waliofariki, ambayo imepokelewa na kuwekwa kwenye uwanja uliopo nje ya Hospitali ya Chuo Kikuu cha Bashair.

Taifa hilo la Sudan, limekumbwa na ghasia tangu Aprili 2023, baada ya mapigano kuzuka kati ya jeshi la Serikali linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah Burhan na vikosi vya Rapid Support Forces – RSF, vinavyoongozwa na Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo.

Tuhuma za Mikutano: Lissu, Mbowe watoa kauli
Rais Samia adhamiria kuimarisha huduma ya Maji