Ndege binafsi iliyokuwa inaruka kutoka katika eneo la hotel moja ya kifahari nchini Msumbiji imeanguka na kujeruhi vibaya watu saba kati ya nane waliokuwa ndani.

Ndege hiyo ilikuwa inatoka kisiwa cha Bazaruto ambako kuna hotel ya kifahari inayogharimu zaidi ya $2300 kwa usiku mmoja

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Mamlaka ya Anga nchini Msumbiji, Joao de Abreu upelelezi juu ya tukio hilo unaendelea na wanamshikilia rubani wa ndege hiyo ndogo.

“Huenda ikawa imetokana na hali ya hewa, lakini tunaendelea kufanya uchunguzi. Niseme tu kuwa rubani wa ndege tunamshikilia kwa mahojiano na vibali na nyaraka zote za ndege hiyo vimeshikiliwa pia,” alisema de Abreu.

Kwa mujibu wa BBC, majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya nchi jirani ya Afrika Kusini.

Mohamed Salah abeba tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka 2017
Mama, watoto wateketea kwa moto ajali ya Treni