Serikali ya Tanzania imezuia ndege za Kenya Airways (KQ) kutua nchini kufuatia barua iliyosomwa na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Hamza Johari Julai 31,2020.
Hatua hiyo imekuja baada serikali ya Kenya kuitenga Tanzania katika Orodha ya mataifa yatakayo ruhusiwa kuingiza ndege zao nchini humo.
”Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imebaini kupitia vyombo vya habari kutengwa kwake ndani ya orodha ya nchi ambazo watu wao wataruhusiwa kwenda Kenya kuanzia Agosti 1, 2020 tarehe ambayo Kenya itafungua Anga lake kwa safari za kimataifa tangu iliposimamisha machi 25,2020” imeelza taarifa ya TCAA
Waziri wa Usafirishaji Kenya James Macharia Julai 31,2020 alitaja orodha ya mataifa 11 ambayo raia wake wataruhusiwa kuingia nchini humo ambazo ni China ,korea Kusini, Japan, Canada, Zimbabwe, Ethiopia, Switzerland, Uganda, Rwanda, Namibia na Morocco kwa maelezo kuwa yamefanikiwa kudhibiti kasi ya maambukizi ya Covid 19.
Hata hivyo waziri Macharia amesema serikali ya Kenya inaendelea kufuatilia kwa ukaribu mataifa mengine kwaajili ya kuongeza idadi ya mataifa mengine yatakayoruhusiwa kuingia nchini humo.