Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi, amewataka Wamiliki wa mashamba ya mradi wa kilimo cha umwagiliaji zabibu wametakiwa kujitokeza kuyafufua mashamba hayo katika msimu wa kilimo kwa sababu kukutakuwa na uhakika wa soko.
Ndejembi ametoa wito huo alipotembelea mashamba ya mradi wa kilimo cha zabibu yaliyoko kijiji cha Chinangali wilaya ya Chamwino ,pia amewataka wamiliki wa mashamba hao kujitokeza kuyafufua katika msimu wa kilimo kwa sababu serikali imeweka miundombinu ya uhakika wa soko la zao hilo.
“Ndugu zangu wawakilishi wa wakulima mliopo hapa nimeamua kuanza na mradi huu wa zabibu. Najua mradi huuulianza vizuri, lakini kwa miaka kadhaa umesuasua. Nawaomba mkawajulishe na wengine tuhakikishe tunafufuamradi wetu,” amesema Ndejembi.
Amesema nia yake ni kuhakikisha mradi huo wa kilimo cha zabibu unafufuliwa kwa sababu serikali imeandaa mazingira mazuri na uhakika wa soko na kwamba ulikuwa unatoa ajira kwa makundi ya vijana na kinamama hasa wakati wakuanza kilimo mpaka kuvuna.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Kenneth Yindi, amesema mradi huo ulianzishwa mwaka 2008 na kuna mashamba yenye ukubwa wa ekari 250 yaliyopandwa zabibu.
Yindi amesema mradi huo ulianza kusuasua tangu mwaka 2015 baada ya baadhi ya wakulima kupokea mkopo wa Sh.bilioni 1.6 kutoka benki ya CRDB.
Amebainisha kuwa wakulima hao hawakupata elimu ya matumizi ya fedha hizo jambo ambalo lilisababisha kuzitumia njeya malengo yaliyokusudiwa na kuyakimbia mashamba