Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC wanahusishwa na taarifa za kuwa mbioni kumuajiri Kocha kutoka nchini Senegal Lamine Ndiaye, ambaye alikua miongoni mwa walioomba kazi klabuni hapo.

Simba ilifungua dirisha la maombi ya kazi, baada ya kuachana na Kocha Didier Gomes mwishoni mwa mwezi Oktoba, kufuatia kikosi chao kuondoshwa kwenye Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Taarifa zinasema kuwa, Ndiaye anayekinoa kikosi cha AC Horoya ya Guinea, anapewa nafasi kubwa ya kuwa Mkuu wa Benchi la Ufundi la Simba SC.

Ndiaye amewahi kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika akiwa na TP Mazembe ya DR Congo, na amepata mafanikio ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya DR Congo, Sudani na Guinea.

Wakati Simba ikihusishwa na mchakato wa kumtangaza Ndiaye, inadaiwa kuwa Uongozi wa klabu hiyo umefuta uwezekano wa kumuajiri Kocha wa Mamelodi Sandowns ya Afrika Kusini Rulani Mokwena kutokana na matakwa yake ya kimasilahi kuwa makubwa kuliko uwezo wa klabu.

Kwa mujibu wa takwimu za gharama za Mokwena kwenye miaka ya hivi karibuni, Simba ilipaswa kutenga kiasi kisichopungua Sh 1.2 bilioni kwa mwaka kwa ajili ya kumlipa mshahara, fedha ambayo haijumuishi posho, bonasi na stahiki nyingine ambazo zikijumuishwa angeweza kuigharimu zaidi ya Sh 1.3 bilioni kwa mwaka.

Kwa mujibu wa vyombo mbalimbali vya habari huko Afrika Kusini, mshahara wa mwezi kwa Mokwena hivi sasa ni kiasi cha Randi 650,000 ambacho ni takribani Shilingi 98 milioni kwa thamani ya fedha ya Tanzania.

Hii inamaanisha kuwa kwa miezi 12, Simba ilipaswa kumlipa Mokwena kiasi cha Sh 1.17 bilioni kwa ajili ya mshahara tu.

Lakini kana kwamba haitoshi, Simba ingelazimika kulipa kiasi kikubwa cha fedha takribani Dola 260,000 (zaidi ya Sh 600 milioni) ili kuvunja mkataba wa Mokwena mwenye umri wa miaka 34.

Album ya Harmonize yafanya maajabu chini ya masaa 10
Kanye West na Big Sean bifu lanukia.